Ufunuo wa Yohana 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 19 (Swahili) Revelation 19 (English)

Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu. Ufunuo wa Yohana 19:1

After these things I heard something like a loud voice of a great multitude in heaven, saying, "Hallelujah! Salvation, power, and glory belong to our God:

kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake. Ufunuo wa Yohana 19:2

for true and righteous are his judgments. For he has judged the great prostitute, who corrupted the earth with her sexual immorality, and he has avenged the blood of his servants at her hand."

Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele. Ufunuo wa Yohana 19:3

A second said, "Hallelujah! Her smoke goes up forever and ever."

Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya. Ufunuo wa Yohana 19:4

The twenty-four elders and the four living creatures fell down and worshiped God who sits on the throne, saying, "Amen! Hallelujah!"

Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. Ufunuo wa Yohana 19:5

A voice came forth from the throne, saying, "Give praise to our God, all you his servants, you who fear him, the small and the great!"

Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki. Ufunuo wa Yohana 19:6

I heard something like the voice of a great multitude, and like the voice of many waters, and like the voice of mighty thunders, saying, "Hallelujah! For the Lord our God, the Almighty, reigns!

Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Ufunuo wa Yohana 19:7

Let us rejoice and be exceedingly glad, and let us give the glory to him. For the marriage of the Lamb has come, and his wife has made herself ready."

Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing'arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Ufunuo wa Yohana 19:8

It was given to her that she would array herself in bright, pure, fine linen: for the fine linen is the righteous acts of the saints.

Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu. Ufunuo wa Yohana 19:9

He said to me, "Write, 'Blessed are those who are invited to the marriage supper of the Lamb.'" He said to me, "These are true words of God."

Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii. Ufunuo wa Yohana 19:10

I fell down before his feet to worship him. He said to me, "Look! Don't do it! I am a fellow bondservant with you and with your brothers who hold the testimony of Jesus. Worship God, for the testimony of Jesus is the Spirit of Prophecy."

Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Ufunuo wa Yohana 19:11

I saw the heaven opened, and behold, a white horse, and he who sat on it is called Faithful and True. In righteousness he judges and makes war.

Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Ufunuo wa Yohana 19:12

His eyes are a flame of fire, and on his head are many crowns. He has names written and a name written which no one knows but he himself.

Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. Ufunuo wa Yohana 19:13

He is clothed in a garment sprinkled with blood. His name is called "The Word of God."

Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. Ufunuo wa Yohana 19:14

The armies which are in heaven followed him on white horses, clothed in white, pure, fine linen.

Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. Ufunuo wa Yohana 19:15

Out of his mouth proceeds a sharp, double-edged sword, that with it he should strike the nations. He will rule them with a rod of iron. He treads the winepress of the fierceness of the wrath of God, the Almighty.

Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana. Ufunuo wa Yohana 19:16

He has on his garment and on his thigh a name written, "KING OF KINGS, AND LORD OF LORDS."

Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; Ufunuo wa Yohana 19:17

I saw an angel standing in the sun. He cried with a loud voice, saying to all the birds that fly in the sky, "Come! Be gathered together to the great supper of God,{TR reads "supper of the great God" instead of "great supper of God"}

mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa. Ufunuo wa Yohana 19:18

that you may eat the flesh of kings, the flesh of captains, the flesh of mighty men, and the flesh of horses and of those who sit on them, and the flesh of all men, both free and slave, and small and great."

Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake. Ufunuo wa Yohana 19:19

I saw the beast, and the kings of the earth, and their armies, gathered together to make war against him who sat on the horse, and against his army.

Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; Ufunuo wa Yohana 19:20

The beast was taken, and with him the false prophet who worked the signs in his sight, with which he deceived those who had received the mark of the beast and those who worshiped his image. These two were thrown alive into the lake of fire that burns with sulfur.

na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao. Ufunuo wa Yohana 19:21

The rest were killed with the sword of him who sat on the horse, the sword which came forth out of his mouth. All the birds were filled with their flesh.